Kiungo wa Yanga Khalid Aucho jana aliiongoza timu ya Taifa ya Uganda kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Rwanda katika mchezo wa kusaka tiketi ya michuano ya kombe la Dunia
Aucho ndiye nahodha wa timu ya Taifa ya Uganda, kile anachokifanya akiwa na Yanga, anakifanya kwenye timu ya Taifa pia
Daktari huyo wa mpira atarejea nchini kuungana na Yanga baada ya mchezo wa marudiano dhidi ya Rwanda ambao utapigwa keshokutwa Oktoba 10, Uganda
Nyota wa Yanga walio na majukumu ya timu za Taifa, watakamilisha majukumu yao mwishoni mwa wiki hii
ADVERTISE HERE