Kama tulivyotaarifu awali, Yanga imemalizana na Youthe Rostand aliyekuwa mlinda lango namba moja wa African Lyon.
Youthe Rostand amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga, mabingwa wa kihistoria(mara 27) ligi ya soka Tanzania Bara.
Hakuna mwenye shaka juu ya uwezo wa Rostand raia wa Cameroon na bila hiyana tunamtakia kila la kheri Deogratius Munishi 'Dida' ambaye hatutakuwa nae msimu ujao.
Licha ya African Lyon kuteremka daraja, Youthe Rostand alikuwa nguzo muhimu kwa timu hiyo langoni.
Huyu alikuwa miongoni mwa makipa waliofanya vizuri sana msimu uliopita.

ADVERTISE HERE