Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' jioni ya leo itashuka kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Benin katika mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu fainali ya michuano ya kombe la Dunia 2022 itakayofanyika Qatar
Tanzania inaongoza kundi J ikiwa na alama nne huku nafasi ya pili ikishikiliwa na Benin pia yenye alama nne
Timu hizo zinatofautiana katika mabao ya kufunga na kufungwa
Katika mchezo huo ambao CAF imeruhusu mashabiki 10,000; Tanzania inahitaji kushinda lengo likiwa kukusanya alama zote tisa nyumbani
Walipata ushindi dhidi ya Madagascar, wanahitaji kuifunhga Benin na baadae DR Congo ili kujiwekea mazingira mazuri ya kuongoza kundi na pengine kutinga awamu ya mwisho ya mchujo
Kikosi cha Kim Poulsen kiko kamili kikiwajumuisha nyota wote ikiwa ni pamoja na nahodha Mbwana Samatta na winga Saimon Msuva
Mchezo utapigwa kuanzia saa kumi kamili jioni