Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu fainali za kombe la Sunia kati ya Tanzania dhidi ya Benin ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa kesho Alhamisi
Awali kulikuwa na hatihati kuwa mchezo huo ungepigwa pasipo mashabiki, lakini sasa Watanzania watapata fursa ya kuishangilia timu yao pale uwanja wa Benjamin Mkapa
Kwa Tsh 5,000/- tu unaweza kukaa Majukwaa ya VIP B na C wakati Mzunguuko ni Tsh 3,000/- tu
Mchezo utapigwa kuanzia saa kumi kamili jioni
ADVERTISE HERE