Nabi ataka mechi mbili za Kimataifa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Oct 2021
Nabi ataka mechi mbili za Kimataifa

Wakati ligi ikisimama kupisha kalenda ya michuano ya Kimataifa, kikosi cha Yanga kitatumia mapumziko hayo ya Kimataifa kujiweka sawa ambapo Kocha Nasreddine Nabi ametaka atafutiwe michezo miwili ya Kimataifa

Baada ya mchezo dhidi ya Geita Gold, Nabi alisema wanatarajia kuelekea Arusha kuweka kambi maalum kabla ya mchezo dhidi ya KMC

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema wanafanyia kazi mapendekezo ya Mwalimu ambapo wanatafuta mechi hizo mbili moja ikitarajiwa kuchezwa jijini Dar es salaam na nyingine nje ya Jiji

"Ligi itasimama kwa wiki kadhaa, uongozi umepokea mapendekezo ya Mwalimu Nabi ambaye anataka michezo miwili ya Kimataifa. Tunatafuta mechi hizo mbili, mchezo tutacheza hapa Dar es salaam na mwingine tutaucheza nje ya Dar," alisema Bumbuli

Kikosi cha Yanga kinawakosa wachezaji wake nane ambao wanakabiliwa na majukumu ya timu za Taifa

Wachezaji hao ni Ramadhani Kabwili, Kibwana Shomari, Dickson Job, Feisal Salum, Saido Ntibazonkiza, Yacouba Songne, Djigui Diarra na Khalid Aucho

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
7h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
11h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
16h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
20h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’