Kiungo wa Yanga Mukoko Tonombe amemaliza adhabu ya kukosa michezo mitatu kufuatia kadi nyekundu aliyopewa kwenye mchezo wa fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) msimu uliopita dhidi ya Simba
Mukoko amekosa michezo dhidi ya Simba (Ngao ya Jamii), Kagera Sugar na Geita Gold
Mukoko anaweza kurejea kikosini katika mchezo dhidi ya KMC ambao utapigwa Oktoba 19 katika uwanja wa Majimaji, Songea
Hata hivyo mtihani utabaki kwa Kocha Nasreddine Nabi na benchi lake la ufundi kwani sasa safu yake ya kiungo imekamilika
Kuna Yannick Bangala, Khalid Aucho, Mukoko Tonombe na Zawadi Mauya
Nabi anapendelea kutumia viungo wawili nyuma, (4-2-3-1), hivyo kama Bangala hatatumika katika safu ya ulinzi, anaweza kulazimika kubadili mfumo ili kuweza kutumia viungo watatu, kama sivyo kiungo mmoja (Mukoko, Bangala, Aucho) atapaswa kuanzia benchi