Nahodha wa Yanga Bakari Nondo Mwamnyeto ameenguliwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa kutokana na majeraha ya kidole yanayomsumbua
Mwamnyeto alikuwa miongoni mwa wachezaji watano wa Yanga walioitwa timu ya Taifa kwa ajili ya mechi za kuwania kufuzu fainali za kombe la Dunia 2022
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema kutokana na ufinyu wa muda wa maandalizi kuelekea michezo dhidi ya Benin, hakutakuwa na uwezekano wa Mwamnyeto kuweza kutumika katika michezo hiyo kwani bado hayuko tayari kuanza mazoezi na wachezaji wengine
Nyota wanne wa Yanga waliobaki katika kikosi cha Stars ni Ramadhani Kabwili, Kibwana Shomari, Dickson Job na Feisal Salum 'Fei Toto'
ADVERTISE HERE