Baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Geita Gold mwishoni mwa wiki, kikosi cha Yanga leo kinarejea mazoezini kuendelea na maandalizi licha ya kuwakosa baadhi ya wachezaji wanaokabiliwa na majukumu ya timu za Taifa
Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema watatumia siku 15 za mapumziko ya Kimataifa kujiimarisha ili kuhakikisha wanarejea wakiwa imara
Yanga inatarajiwa kuelekea mkoani Arusha kuweka kambi maalum ya maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya KMC utakaopigwa uwanja wa Uhuru, Oktoba 19
"Kesho (leo) tunarudi mazoezini kujiandaa zaidi, tuna muda wa siku 15 tutazitumia kujijenga zaidi na kuimarika zaidi na tutarudi tuko vizuli zaidi," alisema Kaze
Wachezaji ambao wameondoka kwenda kujiunga na timu za Taifa ni Djigui Diarra (Mali), Khalid Aucho (Uganda), Yacouba Songne (Burkina Faso) na Saido Ntibazonkiza (Burundi)
Wengine ni Ramadhani Kabwili, Kibwana Shomari, Bakari Nondo Mwamnyeto, Dickson Job na Feisal Salum walioitwa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'