Mshambuliaji wa zamani wa Yanga Amissi Tambwe anaitumikia klabu ya DTB inayoshiriki ligi daraja la kwanza (Championship)
Tambwe ameanza msimu kibabe kwa kutupia mabao manne katika mchezo dhidi ya African Lyon hapo jana
Mkongwe huyu amedhihirisha bado anayo makali katika kuzifumania nyavu
Tambwe anaweza kurejea ligi kuu katika usajili wa dirisha dogo kama ataendeleza makali yake katika kuzifumania nyavu
Mabao manne katika mchezo wa kwanza ni dalili njema za msimu wenye mafanikio kwake
ADVERTISE HERE