Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amethibitisha kuwa mlinzi Kibwana Shomari ameitwa katika kikosi cha timu ya Taifa kinachojiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la Dunia dhidi ya Benin utakaopigwa Oktoba 07 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Kibwana amekuwa katika kiwango bora ambapo katika msimu huu ametumika kwenye safu ya ulinzi upande wa kushoto
"Tumepokea taarifa ya wito wa Kibwana. Na kwa heshima tumemruhusu akajiunge na timu ya Taifa wakati tukisubiri barua rasmi kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambayo tutaipata Jumatatu, Tunajivunia kuitwa kwake na tunampongeza sana, tunaamini kocha hakufanya makosa katika uteuzi wake kwani ameona kuna kitu kwa kijana wetu," alisema Bumbuli
Baada ya uteuzi wa timu ya Taifa aliofanywa na Kocha Mkuu Kim Poulsen, wengi walihoji kutojumuishwa kwa Kibwana ambaye amekuwa katika kiwango bora ndani ya kikosi cha Yanga
Poulsen amejiridhisha kuwa ni wakati sahihi kumjumuisha Kibwana katika kikosi chake
Kibwana amezitumikia timu zote za Taifa kuanzia ngazi ya vijana U17 na U20
Anaungana Ramadhani Kabwili, Feisal Salum, Bakari Nondo Mwamnyeto na Dickson Job ambao walijumuishwa katika kikosi kilichotangazwa wiki iliyopita