Baada ya mechi za raundi ya pili, ligi kuu itasimama kupisha kalenda ya michuano ya FIFA ambapo mechi za kuwania kufuzu fainali ya michuano ya kombe la dunia zitapigwa
Yanga imetoa takribani wachezaji nane walioitwa kwa ajili ya majukumu ya timu za Taifa
Wachezaji hao ni Ramadhani Kabwili, Bakari Nondo Mwamnyeto, Dickson Job na Feisal Salum walioitwa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'
Wengine ni Djigui Diarra (Mali), Khalid Aucho (Uganda), Saido Ntibazonkiza (Burundi) na Yacouba Songne (Burkina Faso)
ADVERTISE HERE