Wananchiiiiii, tukutane kwa Mkapa, zamu ya Geita Gold

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Oct 2021
Wananchiiiiii, tukutane kwa Mkapa, zamu ya Geita Gold

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa leo katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Geita Gold utakaopigwa kuanzia saa moja usiku

Bumbuli amewaambia Wananchi wajae, watafurahi pia watakuwa na kazi ya kuhesabu pasi za Yanga ili kuhakikisha hakutokeo mambo ya kukisia takwimu baada ya mchezo huo!

Kwa sasa Wananchi wana kila sababu ya kuwa na 'kiburi' kwani wana timu nzuri bhana

Muhimu zaidi ni kuongeza hamasa ili kuhakikisha alama zote tatu zinabaki jijini Dar es salaam

Baada ya kuanza kwa kusuasua katika misimu minne iliyopita, msimu huu Wananchi wameanza kwa ushindi kule Bukoba kwa kuichapa Kagera Sugar bao 1-0

Leo wanahitaji kuendeleza wimbi la ushindi, wakifunga mabao mengi wanaweza kujikuta wako kileleni mwa msimamo wa ligi, nafasi ambayo inashikiliwa na watani zao kwa muda

Msemaji wa Yanga Haji Manara jana aliwaambia wanahabari kuwa kila mchezo kwao una umuhimu mkubwa hivyo hawatawadharau Geita Gold kwa kigezo ni timu iliyopanda daraja

Wanahitaji kushinda mchezo huo katika mpango wa kutimiza malengo waliyojiwekea msimu huu, kutwaa ubingwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
17h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
21h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
22h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’