Msemaji wa klabu ya Yanga Haji Manara amesema wamedhamiria kwelikweli kushinda ubingwa wa ligi kuu msimu huu, hivyo watahakikisha wanafanya vizuri katika kila mchezo unaokuja mbele yao
Kesho Jumamosi Yanga itashuka kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Geita Gold katika mchezo wa ligi kuu utakaopigwa kuanzia saa moja usiku
Manara amesema hawataidharau Geita Gold kwani kwa kuwa miongoni mwa timu zinazoshiriki ligi kuu msimu huu, ni timu nzuri
"Tumejipanga kutwaa ubingwa msimu hivyo kila mchezo kwetu una umuhimu mkubwa. Tunawaheshimua Geita Gold, ni timu nzuri, tutawakabili kwa tahadhari kama tulivyofanya katika michezo iliyopita. Nawaambia mashabiki wa Yanga wawe na imani na timu yao, tumejipanga kwelikweli"
"Tuna timu nzuri yenye wachezaji bora, kina Yannick Bangala, Khalid Aucho, na wengine ambao ni wachezaji wa daraja la juu kabisa. TFF ina bahati sana kwa ligi yetu kupata wachezaji mahiri sana. Katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar niliwafuatilia Bangala na Aucho na kujiridhisha na uwezo wao. Utulivu alionao Bangala kama kuna mtu atanitajia mchezaji katika ligi yetu anayeweza kumfikia basi nitampa Tsh Milioni 1 kila dakika mpaka anakufa!," alitamba Manara
Nae Mkuu wa idara ya Mawasiliano Hassan Bumbuli amesema kuwa kila mchezo ambao wanacheza ni mgumu sana na hivyo lazima wachukulie kwa uzito
Wachezaji na benchi la ufundi wanafahamu kila timu inatamani kushinda mbele ya Yanga ili kujiwekea historia ya kuifunga klabu kubwa
Amesema wachezaji wapo imara na salama kwa ajili ya mchezo wa kesho
Viingilio vya mchezo huo VIP A ni Tsh 15,000/-, VIP B Tsh 10,000 /=- huku Mzunguuko ni Tsh 5,000/-