Jioni ya leo Yanga inashuka uwanjani Kaitaba kuikabili Kagera Sugar katika mchezo wa kwanza ligi kuu msimu huu
Yanga ilitua Kagera juzi ikiwa na kikosi chake kamili kilichopeleka kilio Msimbazi mwishoni mwa wiki iliyopita
Habari ya mjini ni mshambuliaji Fiston Mayele ambaye alifunga bao pekee la Yanga katika mchezo huo
Mayele alipokewa kifalme Kagera akibebwa juu juu na mashabiki waliojitokeza kwa wingi kuipokea timu yao
Ni mapokezi ambayo yamemuongezea 'mzuka' Mayele kuelekea mchezo wa jioni ya leo
Mshambuliaji huyo raia wa DR Congo amesema mashabiki watarajie mambo mazuri kutoka kwake akilenga kufunga kila atakapopata nafasi
"Nafurahi mashabiki wengi wamenipokea vizuri, nawaahidi nitaendelea kuwapa furaha kwa kufunga mabao," alisema Mayele
Mayele leo anatarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji ya Yanga katika mchezo ambao wanahitaji kushinda mbele ya Kagera Sugar