Tuko tayari kuivaa URA - Nsajigwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Jan 2018
Tuko tayari kuivaa URA - Nsajigwa
Kocha Msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa amesema baada ya kumalizika kwa hatua ya makundi, kombe la Mapinduzi kikosi cha Yanga kinajiandaa kuikabili URA kwenye mchezo wa nusu fainali kesho.

Akizungumza baada ya mchezo dhidi ya Singida United jana, Nsajigwa amesema wameridhika na matokeo ya sare ya bao 1-1 licha ya kuwa walijipanga kupata ushindi.

Amesema sasa wanajiandaa kuikabili URA katika mchezo wa nusu fainali Jumatano.

"URA ni timu nzuri, wamewafunga Azam, Simba timu ambazo ni nzuri, tutatumia mapumziko ya siku mbili hizi kujiandaa kukabiliana nao," amesema Nsajigwa.

Nsajigwa ameongeza kuwa Yanga itaendelea kuwatumia wachezaji waliopo kikosini visiwani Zanzibar na haina mpango wa kuongeza wachezaji wengine.

Baada ya kurejea kwa Obrey Chirwa ilitarajiwa mchezai huyo angesafiri kwenda Zanzibar kuongeza nguvu kwenye kikosi cha Yanga.

Hata hivyo Chirwa amewekwa 'kiti moto' na Kamati ya Nidhamu ya Yanga akitakiwa ajieleze kwa nini alichelewa kurudi baada ya kupewa ruhusa kwenda kwao kushughulikia matatizo ya kifamilia.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’