Kikosi cha Yanga jioni ya leo kimekamilisha maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar ambao utapigwa kesho Jumatano katika uwanja wa Kaitaba
Yanga imefanya mazoezi yake ya mwisho katika uwanja huo ambao utatumika siku ya kesho kuanzia saa kumi jioni
Msemaji wa Yanga Haji Manara amesema wachezaji wote waliosafiri nao Bukoba wako katika hali nzuri isipokuwa nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto ambaye amepata maumivu katika kidole chake
ADVERTISE HERE