Ligi Kuu ya Tanzania Bara imeendelea leo kwa michezo mitatu kupigwa katika viwanja mbalimbali
Kule Musoma, Wanajeshi wa Mpakani Biashara United 'wamechezea sharubu za Mnyama' baada ya mchezo dhidi ya Simba kumalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana
Simba walipewa 'tuta' kwenye dakika za majeruhi lakini, hawakuweza kuutumbukiza mpira kambani
Mbeya City wao wamepata ushindi wa bao 1-0 dakika za majeruhi dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo uliopigwa uwanja wa Sokoine
Mapema Dodoma Jiji waliilaza Ruvu Shooting bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Jamhuri, Dodoma
Yanga watakuwa uwanjani kesho Jumatano katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar ambao utapigwa uwanja wa Kaitaba, Bukoba
Wananchi wanahitaji ushindi wa zaidi ya mabao mawili ili kuwaondoa Namungo Fc kileleni mapema kabisa!
Hakika utakuwa ni mchezo wa fainali kwa Yanga, kuhakikisha wanazipata alama zote tatu