Wakati Wananchi wakitarajiwa kushuka dimbani kesho Jumatano kuikabili Kagera Sugar kule mkoani Kagera, mikiki mikiki ya ligi kuu inaendelea leo kwa michezo mingine mitatu kupigwa
Mchezo wa mapema saa nane ni kati ya Dodoma Jiji dhidi ya Ruvu Shooting ukipigwa uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma
Dabi ya Mbeya inapigwa leo, ambapo Mbeya City itaumana na Tanzania Prisons katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya kuanzia saa kumi jioni
Wanajeshi wa mpakani, Biashara United wao watakuwa wenyeji wa Simba katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Karume
Jana Mbeya Kwanza waliichapa Mtibwa Sugar bao 1-0, Coastal Union ikatoshana nguvu na Azam Fc kwa sare ya bao 1-1 wakati Namungo Fc waliichapa Geita Gold mabao 2-0

ADVERTISE HERE