Khalid Aucho ni kiungo aliyekamilika, anaisaidia timu katika nyakati zote, wakati ikiwa na mpira na hata bila ya mpira
Anatawala dimba, anaweza kuamua timu icheze kwa namna gani, timu ikiwa kwenye presha anatuliza, kukiwa na uhitaji wa kwenda kushambuliaji anaanzisha mashambulizi
Kiungo mgumu asiye na haraka lakini mambo yake ni ya uhakika
Jana katika mchezo dhidi ya Simba, aliongoza kwa kupiga pasi ambapo katika pasi 42, iliyoharibika ni moja tu
Huyu sasa ndio 'Magician left footer', kiungo aliyekamilika
Kwa kiwango alichoonyesha jana tena ukiwa mchezo wake wa kwanza, sambamba na Yannick Bangala, Kocha Nasreddine Nabi ana kazi ya kuamua pacha ipi aitumie kwani nje anao Mukoko Tonombe na Zawadi Mauya
Lakini kwa hakika Mukoko na Mauya wana kazi ya kufanya kuwapindua Aucho na Bangala katika eneo la kiungo kama Nabi ataendelea kutumia viungo wawili wakabaji