Mchezo wa kukamilisha ratiba kati ya Yanga dhidi ya Singida United umemalizika kwa sare ya bao 1-1 na hivyo kuiwezesha Singida United kumaliza ikiwa kileleni mwa kundi B.
Timu zote zimemaliza zikiwa na alama 13, Singida United ikiizidi Yanga kwa tofauti ya mabao.
Timu zote ziliingia kwenye mchezo huo kwa nidhamu ya hali ya juu. Hata upatikanaji wa mabao kwa kila upande umetokana na makosa ya walinzi katika kuzuia mipira ya adhabu.
Mabao yote yamepatikana kwenye kipindi cha pili Danny Lyanga akifunga bao la Singida United baada ya kuunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu huku Said Juma Makapu akifunga bao la Yanga kwenye dakika za majeruhi nae akiunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu uliopigwa na Ibrahim Ajib.
Yanga sasa itachuana na URA keshokutwa Jumatano katika mchezo wa nusu fainali huku Singida United ikitarajiwa kukabiliana na Azam Fc kwenye mchezo mwingine wa nusu fainali siku hiyohiyo.
Kwa mara nyingine kikosi cha Yanga kimeonyesha utayari wa kupambana na timu yoyote bila kujali kinawakosa wachezaji gani.
Wengi walidhani Singida United iliyosheheni 'maproo' ingeweza kuifunga kirahisi Yanga iliyosheheni vijana zaidi na 'pro' mmoja, Youthe Rostand.

ADVERTISE HERE