Mshambuliaji Fiston Mayele ameendeleza moto wake wa kuzifumania nyavu katika michezo ya kirafiki jana akifunga moja ya mabao ya Yanga katika mchezo wa kirafiki dhidi ya DTB
Katika mchezo huo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-1, Kocha Nasreddine Nabi aliwatumia wachezaji ambao hawakutumika katika michezo dhidi ya Rivers United na wale waliopata dakika chache
Mabao mengine ya Yanga yalifungwa na mlinzi wa kushoto David Bryson na Yusufu Athuman
Mayele sasa amefunga mabao manne katika mechi za kirafiki zilizopigwa Avic Town, Kigamboni
ADVERTISE HERE