Yanga itajilaumu kwa kukosa matokeo katika mchezo wa kwanza dhidi ya Rivers United ambao ulipigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Kile kilichotokea Nigeria juzi, ni funzo kwa viongozi wetu, wafahamu wanapokuwa nyumbani ni vita, lazima matokeo yapatikane kwa gharama yoyote
Watanzania uungwana ni asili yetu lakini hao tunaowathamini wakija kucheza kwetu, tukienda kwao hawana habari na sisi
Rivers United walitumia kila mbinu nje na ndani ya uwanja kuhakikisha wanapata matokeo
Sisi hilo hatukulifanya nyumbani, wakati mwingine tunapaswa kuwa na roho ya kikatili kidogo
Haimaanishi wakija tuwapige, la hasha bali tuwatengenezee mazingira ambayo yatawavuruga kisaikolojia kama wanavyotufanyia tukienda kwao
Walichofanya Rivers United ni kutuondoa mchezoni kwa kusingizia wachezaji wana covid, kutofungua vyumba vya kubadilishia nguo kwa wakati na kuondoa taa zote katika vyumba wakisingizia umeme hamna
Waliwasumbua maafisa wa Yanga nje ya uwanja kuhakikisha hawapati utulivu muda wote
Ilikuwa ni marufuku kwa yeyote katika msafara wa Yanga kushika simu yake ndani ya uwanja. Kwa kuwa hawakutaka yale wanayoyafanya yafahamike huko nje...!
Kwa wenzetu mechi zao za nyumbani ni vita lakini sisi huku ni tofauti