Safari ya Yanga katika michuano ya ligi ya mabingwa imefika ukingoni kabla ya kuanza mbele ya Rivers United
Ni baada ya kupoteza michezo yote miwili ya nyumbani na ugenini kwa kufungwa bao 1-0
Ni matokeo yaliyowaumiza wengi pamoja na kuwa changamoto zilizopelekea Yanga kutokufanya vizuri zina mashiko
Hakuna muujiza kupata mafanikio kwenye mpira wa miguu. Pamoja na mipango mizuri, timu inahitaji maandalizi
Yanga ina wachezaji wazuri, benchi bora la ufundi lakini kuelekea mechi za ligi ya mabingwa, haikuwa na maandalizi ya kutosha kutokana na ufinyu wa muda
Mpaka sasa mashabiki wa Yanga bado hawajashangilia ushindi kutoka kwa kikosi chao kilichosukwa upya
Hakukuwa na matokeo mazuri katika mchezo wa wiki ya Mwananchi na hali imekuwa hivyo katika mechi mbili za ligi ya mabingwa dhidi ya Rivers United
Hapa utaona umuhimu wa Yanga kupata ushindi katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumamosi ijayo
Ni hivi, ushindi katika mchezo huo utakiweka kikosi cha Yanga tayari kwa mikiki mikiki ya ligi kuu ambapo Wananchi wataanzia mkoani Kagera Septemba 29
Baada ya kuondoshwa ligi ya mabingwa, mashabiki wa Yanga wanataka kushinda Ngao ya Jamii, ubingwa wa ligi kuu, ubingwa wa FA na kombe la Mapinduzi
Kwa kocha Nasreddine Nabi, huu ni mchezo ambao anahitaji kushinda ili kuondoa presha ya mashabiki ambao tayari wameanza manun'guniko
Msimu huu Yanga ina timu nzuri, watu wanataka kuona tafsiri ya ubora wa timu kwa kuona matokeo mazuri uwanjani
Matokeo hayo yaanze kuonekana mchezo wa Ngao ya Jamii