Katika mchezo dhidi ya Rivers United uliopigwa Nigeria na Yanga kufungwa bao 1-0 jana, Kocha Nasreddine Nabi alimtumia Yannick Bangala nafasi ya kiungo mkabaji akichukua majukumu ya Zawadi Mauya
Bangala ni mmoja wa wachezaji walion'gara katika mchezo huo akiiongezea Yanga uimara kwenye eneo la kiungo
Kocha Nasreddine Nabi alieleza kuvutiwa na kiwango kilichoonyesha akiamini atakuwa na msaada mkubwa msimu huu
Pengine Nabi amejilaumu kwa kutomtumia katika mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar es salaam
Bangala ni mchezaji kiraka anayemudu kucheza nafasi ya kiungo, mlinzi wa kati au pembeni
Huyu ni mtu wa kazi kwelikweli
ADVERTISE HERE