Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema wamekubali matokeo baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Rivers United kwa kufungwa bao 1-0 jana
Nabi amesema zipo sababu kadhaa ambazo zimechangia wao kutofanya vizuri lakini amesema sasa wanarejea nyumbani wakiwa kamili wakilenga kuanza kwa ushindi kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumapili ijayo
"Tumekuwa na changamoto nyingi, zaidi maandalizi yetu hayakuwa mazuri kutokana na sababu ambazo ziko nje ya uwezo wetu. Tumewakosa baadhi ya wachezaji wetu kutokana na vibali vyao kuchelewa"
"Tumecheza vyema hapa Nigeria, nadhani hatukustahili kupoteza mchezo, tulitengeneza nafasi, tumenyimwa mikwaju ya penati lakini ndio mpira wa miguu ulivyo"
"Sasa tunarejea tukiwa imara, wachezaji ambao hatukuweza kuwatumia katika michuano hii wanarudi kikosini na nafikiri watatuongezea nguvu, tuna nafasi ya kushinda Jumapili," alisema Nabi
Yanga imerejea nchini mapema leo wakitoka Nigeria na moja kwa moja timu kuelekea kambini