Chama kuzikwa kesho Jumanne, Yanga yaomboleza

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Jan 2018
Chama kuzikwa kesho Jumanne, Yanga yaomboleza
Uongozi wa Yanga umeeleza kusikitishwa na kifo cha mchezaji wake wa zamani Athumani Juma Chama maarufu kama 'Jogoo' aliyefariki katika Hospitali ya Muhimbili usiku wa kuamkia leo.

Akituma salamu za ramirambi kwa niaba ya Yanga, Katibu Mkuu Charles Mkwasa amesema Yanga imesikitishwa na kifo cha mkongwe huyo aliyewahi kutamba katika klabu hiyo miaka ya nyuma.

Amewataka wapenzi na wanachama wa Yanga kuungana pamoja na familia ya marehemu Chama katika kipindi hiki kigumu.

Taratibu za mazishi zinafanyika nyumbani kwa marehemu Yombo Mwisho jijini Dar es salaam ambapo anatarajiwa kupumzishwa kwenye nyumba yake ya milele kesho Jumanne katika makaburi ya Kisutu saa saba mchana baada ya kuswaliwa katika msikiti wa Manyema.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’