Bado mpaka sasa Yanga haijapokea majibu ya vipimo vya corona vya wachezaji kuelekea mchezo dhidi ya Rivers United utakaopigwa saa chache zijazo
Mwenyekiti wa DRFA, Lameck Nyambaya amesema hadi sasa bado majibu ya vipimo vya uviko-19 hayajatolewa na Serikali ya Nigeria, hata hivyo wachezaji wote wako sawa, tayari kwa mchezo huo
Katika hatua nyingine, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Saad Khimji amesema morali ya wachezaji iko juu akiwatoa hofu mashabiki wa Yanga nchini kuwa leo itakuwa siku ya furaha kwao
"Wachezaji wamepata muda wa kufanya mazoezi, wamepumzika na muda sio mrefu tunakwenda kujiandaa tayari kuelekea uwanjani. Viongozi tumejipanga, tumepewa sapoti nzuri na wenzetu tuliowakuta hapa Nigeria. Nikwambie tu tuko tayari kuipigani timu yetu na Tanzania kwa ujumla, leo litatokea jambo la kustaajabisha hapa," alisema Khimjiย