Kukosekana kwake katika mchezo uliopigwa jijini Dar es salaam kuliwaibua mashabiki na wadau wa soka kuhoji kwa nini hakuonekana uwanjani
Ni Yannick Bangala Litombo mlinzi wa kati mahiri ambaye anamudu vyema kucheza eneo la kiungo cha ukabaji
Hakuwa na muda mrefu wa kufanya mazoezi na wenzake pengine ndio sababu iliyomfanya kocha Nasreddine Nabi kumuweka nje katika mchezo uliopigwa jijini Dar es salaam dhidi ya Rivers United

Bangala alikuwa miongoni mwa wachezaji walioitwa timu ya Taifa ya DR Congo na alijiunga na kikosi cha Yanga siku mbili kabla ya mchezo dhidi ya Rivers United
Kuelekea mchezo wa marudiano kule Nigeria, Yannick anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kitakachoshuka uwanjani pale Adokiye
Amejifua na wenzake kwa takribani wiki moja, kwa mchezaji wa kiwango chake hahitaji muda mrefu kuzielewa mbinu za kocha wake
Nabi anaweza kumtumia kama mlinzi wa kati au kiungo mkabaji kuilinda safu ya ulinzi
Wananchi wana imani kubwa kwa kikosi chao, bila shaka wachezaji wataweza kufanya kile wanachokitaraji, kurejea nchini na ushindi