Yanga itasafiri kuelekea Nigeria kesho Ijumaa kwa ajili ya mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Rivers United
Mchezo huo utapigwa Jumapili, Septemba 19 huko Nigeria
Ili kuweza kuvuka hatua hii ya awali, Yanga inahitaji kuibuka na ushindi wa kuanzia mabao mawili
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi anapaswa kuingia kwenye mchezo huo kwa lengo ya kushambulia zaidi
Rivers United wana mtaji wa bao la ugenini hivyo ni wazi watacheza kwa tahadhari lakini kwa Yanga matokeo tofauti na ushindi hayatakuwa na maana
Unaweza kuwa mchezo ambao hautakuwa na nafasi nyingi, ushindi unaweza kuamuliwa kupitia nafasi chache zitakazopatikana
Mipira ya kona, adhabu inaweza kuamua, hapa unaweza kuona umuhimu wa mchezaji kama Saido Ntibazonkiza

Saido ni mahiri katika mipira ya adhabu na hata kona, hasa kwa uwepo wa Heritier Makambo ambaye ni mzuri katika mipira ya kichwa
Pia Saido ni mchezaji mwenye uzoefu mkubwa, amecheza mechi za aina hii nyingi. Hii ni silaha muhimu ambayo pengine kama itatumika, inaweza kuinufaisha Yanga
Jambo la uhakika ni kuwa Wananchi watarajie mabadiliko katika kikosi kilichocheza mchezo wa kwanza, Yannick Bangala, Deus Kaseke, Saido wanaweza kujumuishwa katika mchezo huo