Yanga itaondoka kesho Ijumaa kuelekea Nigeria kwa ajili ya mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Rivers United ambao utapigwa Jumapili, Septemba 19
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema msafara wa Yanga utajumuisha takribani watu 80, wachezaji, benchi la ufundi, viongozi na mashabiki ambao watapata fursa ya kwenda kuishangilia timu
Leo wachezaji wanatarajiwa kufanyiwa vipimo vya uviko-19 hapa nchini
Akizungumzia maandalizi ya timu, Bumbuli amesema benchi la ufundi chini ya Kocha Nasreddine Nabi, wamefanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika mchezo uliopita hivyo wana matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika mchezo wa marudiano huko Nigeria
Yanga itaondoka nchini na 'dege' la AirTanzania na itarejea Jumapili baada ya mchezo
ADVERTISE HERE