Wananchi wanasema 'The Return Of Champions' maana yake itatimia baada ya mchezo dhidi ya Rivers United ambao utapigwa Jumapili, Septemba 19 nchini Nigeria
Yanga imedhamiria kwenda kupambana Nigeria kuhakikisha inashinda mchezo dhidi ya Rivers United na kutinga raundi ya kwanza
Huu ni mchezo ambao Kocha Nasreddine Nabi pamoja na vijana wake wanafahamu thamani ya ushindi ambao wanaweza kuupata
Kitendo cha Mfadhili wa Yanga, Ghalib Said Mohammed kukodi AirBus kuwapeleka Wachezaji na Ndege hiyo kuwasubiri kuwarejesha nchini, ni heshima kubwa na uongozi umeonyesha kuwa na imani wanaweza kufanya jambo huko
Yanga haina cha kupoteza nchini Nigeria, wanachotafuta ni matokeo ya ushindi tu hivyo ni mchezo ambao Nabi anafahamu, anahitaji kushambulia kwa muda wote
Mchezo huu utakuwa vita kamili, kutokana na kauli zilizotolewa na maafisa wa Rivers United, Yanga inahitaji kushinda kwa gharama yoyote