Yanga yajipanga kukwepa hujuma Nigeria

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Sep 2021
Yanga yajipanga kukwepa hujuma Nigeria

Baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Rivers United kwa kufungwa bao 1-0 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, viongozi wa Yanga wamegoma kuona timu inaondolewa mashindanoni kirahisi hivyo na sasa nguvu zote zimeelekezwa katika mchezo wa marudiano utakaopigwa nchini Nigeria Septemba 19

Ili kuhakikisha wanaepuka changamoto za aina yoyote kutoka kwa wenyeji wao Rivers United, Yanga tayari imemtanguliza nchini Nigeria Kaimu Mtendaji Mkuu Senzo Mazingisa kwa ajili ya kuandaa mapokezi ya kikosi

Yanga imepenyezewa taarifa kuwa Rivers United wana tabia wa kuwaandalia wapinzani wao mazingira magumu hivyo Senzo atahakikisha anaweka sawa makazi ambayo timu itafikia ikiwa ni Hoteli pamoja na eneo la kufanya mazoezi

Yanga pia itasafiri Nigeria ikiwa kamili, ikibeba chakula, maji na mpishi ambaye ndiye anayewapikia wachezaji kambini Avic Town

Yanga imeuchukulia mchezo wa marudiano dhidi ya Rivers United kama fainali

Kwa hakika zitakuwa dakika 90 za 'machozi, jasho na damu'

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
23m ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
18h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’