FT : Yanga 1-0 Zimamoto

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Jan 2018
FT : Yanga 1-0 Zimamoto
Yanga imeendeleza rekodi yake ya ushindi kwa asilimia 100 baada ya kuilaza Zimamoto bao 1-0 katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Amani Jumapili usiku.

Bao pekee la Yanga liliwekwa kimiani na nyota wa mchezo huo Emanuel Martin aliyeunganisha vyema kwa kichwa krosi ya Juma Mahadhi aliyecheza winga ya kulia.

Yanga iliuanza taratibu mchezo huo hata hivyo mabadiliko yaliyofanywa na benchi la ufundi kwenye kipindi cha pili kwa kuwaingiza Ibrahim Ajib, Raphael Daudi, Pato Ngonyani, Juma Mahadhi na Yohana Nkomola yalibadili kabisa sura ya mchezo huo, Yanga ikitawala kila idara.

Huo ni ushindi wa nne kwa Yanga kwenye michuano hiyo ikiendelea kuwa nyuma ya Singida United kwa tofauti ya mabao. Timu zote zimeshafuzu hatua ya nusu fainali.



Yanga na Singida United zitachuana kesho Jumatatu kwenye mchezo ambao utabainisha mshindi wa kwanza na wa pili.

Mchezo huo utapigwa saa mbili na robo usiku baada ya mchezo wa Simba dhidi ya URA utakaoanza saa kumi kamili jioni.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
57m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’