Yanga imekosa bahati katika mechi za nyumbani Kimataifa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Sep 2021
Yanga imekosa bahati katika mechi za nyumbani Kimataifa

Ni misimu kadhaa Yanga imeshindwa kupata ushindi katika michuano ya ligi ya mabingwa inapocheza nyumbani katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Matokeo ya jana kufungwa bao 1-0 dhidi ya Rivers United, ni mwendelezo wa Yanga kushindwa kutumia uwanja wa nyumbani kwenye michezo ya Kimataifa

Tangu msimu wa 2016/17, Yanga haijashinda mechi zake za ligi ya mabingwa zilizopigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Katika msimu huo walilazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Zanaco Fc ya Zambia na baadae kwenda kutolewa kule Zambia kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana

Msimu uliofuata wakacheza na Township Rollers hapo kwa Mkapa Yanga wakalala kwa mabao 2-1 na baadae kulazimisha suluhu ya bila kufungana kule Botswana

Msimu wa 2019/20 Yanga ikacheza tena na Township Rollers katika uwanja wa Benjamin Mkapa na kulazimishwa sare ya bao 1-1 na baadae kwenda kupata ushindi wa bao 1-0 kule Botswana

Ni katika msimu huohuo wakakutana na Zesco United katika mchezo wa raundi ya kwanza uliopigwa jijini Dar es salaam ukamalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 na Yanga kupoteza kule Zambia kwa kufungwa mabao 2-1

Wakashuka michuano ya Shirikisho wakapangwa na Pyramids, wakaupeleka mchezo jijini Mwanza lakini bado Yanga ikafungwa mabao 2-1 na kule Misri ikafungwa mabao 3-0

Ushindi katika mechi za nyumbani kwa Wananchi katika mechi za Kimataifa limekuwa jambo gumu tangu mwaka 2016

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’