Kocha wa zamani wa Yanga Mwinyi Zahera amerejea Yanga sasa akipewa majukumu ya soka la Vijana
Zahera amerejea akikabidhiwa majukumu ya Mkurugenzi wa Maendeleo ya Soka la Vijana. Amesaini mkataba wa miaka miwili
Wakati akikinoa kikosi cha Yanga, Zahera alikuwa akiwaamini vijana katika timu yeye akiwapandisha kikosini wachezaji kadhaa akiwemo Paulo Godfrey 'Boxer'
Katika mkakati ya Yanga kuunda Taasisi imara ambayo itakuwa na timu zilizojitosheleza kuanzia ngazi ya Vijana, uongozi wa Yanga umemuona Zahera kama mtu sahihi wa kupewa majukumu ya kusimamia timu hizo za vijana
ADVERTISE HERE