Mkurugenzi wa Sheria klabu ya Yanga Simon Patrick ametoa ufafanuzi kilichopelekea wachezaji watatu wa Yanga kuwa na hatihati ya kukosa mechi za awali ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya ITC zao kuchelewa
Simon amewahakikishia Wanayanga kuwa pamoja na uwezekano wa kukosa mechi hizo za awali, Djuma Shabani, Fiston Mayele na Khalid Aucho wana sifa za kushiriki michuano yote ya ndani kwa kuwa ITC zao ziliwasili kabla ya dirisha la usajili wa ndani (TFF) halijafungwa
ADVERTISE HERE