Ukiona watu wanashangilia sana kuwa mchezaji fulani hachezi, ujue wanamuogopa!
Mwamba Djuma Shabani anaweza kukosa mchezo dhidi ya Rivers United baada ya ITC yake kuchelewa lakini haimaanishi kuwa sio mchezaji wa Yanga!
Akikosa mchezo dhidi ya Rivers, wapo wachezaji wengine ambao watacheza nafasi yake
Djuma, kina Khalid Aucho na Fiston Mayele watacheza mechi nyingine zote za Yanga isipokuwa hizi za awali ligi ya mabingwa tu
Septemba 25 watakuwa uwanjani kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba na Septemba 29 watakuwa uwanjani pale ligi itakapoanza!
Sasa kuna watu inabidi wajiandae 'kisaikolojia' kwani wanaweza kuwa wa kwanza kuonja 'shubiri' ya kikosi cha Yanga msimu huu
Hiyo Septemba 25 kuna watu maji wataita 'mma....!', Uwanja wa Benjamin Mkapa hautatosha...!