Kulekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Rivers United ambao utapigwa Jumapili Septemba 12 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Yanga imekuja na kaulimbiu ya "The Return of Champions" yaani Kurejea kwa mabingwa
Msemaji wa Yanga Haji Manara amewataka mashabiki kuhamasishana na kujitokeza kwa wingi pale uwanja wa Mkapa kuhakikisha ushindi unapatikana
Hata hivyo Yanga bado haijapokea taarifa kutoka CAF kuhusu idadi ya mashabiki ambao wataruhusiwa kushuhudia mchezo huo uwanjani
Taarifa kuhusu viingilo na idadi ya mashabiki watakaoruhusiwa, itatolewa baadae
"Mpaka sasa hatujapokea taarifa rasmi kuhusu idadi ya mashabiki ambao wataruhusiwa kuingia uwanjani, taarifa zaidi tutaitoa baadae"
"Hata hivyo tunataka kuona kwa idadi yoyote ya mashabiki watakaoruhusiwa, tunahanikiza vya kutosha uwanjani ili kuwapa ari wachezaji wetu tuweze kuibuka na ushindi mnono"
"Kesho nitakutana na vikundi vyote vya hamasa kuhakikisha hatuendi kunyamaza uwanjani. Tunakwenda kushinda mchezo huu Inshallah," alisema Manara
Manara amesema Yanga imedhamiria kuvuka hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa huku ikilenga kushinda makombe yote ya ndani
Hiyo ndio maana halisi ya kauli mbinu THE RETURN OF THE CHAMPIONS