Pamoja na kuanza mazoezi, mlinzi wa kushoto wa Yanga Yassin Mustafa bado hana utimamu wa asilimia 100 akithibitisha kuwa hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachoikabili Rivers United Jumapili
Yassin alipata changamoto kubwa ya majeraha katikati ya msimu uliopita na hivyo kukosa michezo yote ya duru ya pili
Yassin amesema anaendelea na program maalum ya mazoezi chini ya kocha wa viungo
"Bado sipo sawa kwa asilimia 100, naendelea na mazoezi mepesi chini ya kocha wa viungo, ni wazi sitaweza kucheza dhidi ya Rivers United ila naamini wachezaji waliobaki watatuwakilisha vizuri kutokana na hali waliyonayo," alisema Yassin
Yanga pia huenda ikamkosa mlinzi mwingine wa kushoto David Bryson ambaye amesajiliwa kutoka klabu ya KMC
Bryson ameanza mazoezi hivi karibuni akitoka kwenye majeruhi