Nabi anataka 'mvua' ya mabao

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Sep 2021
Nabi anataka 'mvua' ya mabao

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi anaendelea kukisuka kikosi chake kule Avic Town Kigamboni kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Rivers United ambao utapigwa Jumapili Septemba 12, 2021 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Baada ya mchezo wa wiki ya Mwananchi, Nabi ametumia wiki moja kukiweka sawa kikosi chake ambapo mpaka sasa wako tayari kuikabili Rivers United

Kocha huyo raia wa Tunisia amepania kufanya vizuri katika mchezo wa nyumbani akihitaji washambuliaji wake kufunga mabao mengi

Katika michezo miwili ya kirafiki ambayo Yanga wamecheza baada ya wiki ya Mwananchi, wamefunga mabao manne na kuruhusu bao moja

Akizungumza kwa niaba ya kocha Nabi, Meneja wa Yanga Hafidhi Salehe amesema maandalizi yao yamekamilika kwa kiasi kikubwa na anachokifanya kocha hivi sasa ni kuimarisha safu yao ya ushambuliaji ili kuzitumia nafasi wanazotengeneza

"Tumekuwa na maandalizi mazuri tangu kumalizika wiki ya Wananchi, tumefanya mazoezi ya kutosha na mechi mbili za kirafiki, zimemsaidia kocha kupata picha halisi ya kikosi chake kuelekea mchezo uliombele yetu"

"Karibu idara zote zipo sawa ulinzi na hata kiungo, kocha anaendelea kufanyia kazi eneo la umaliziaji lengo ni kufunga mabao mengi zaidi," alisema Hafidh

Nyota wa Kimataifa wanarejea

Habari njema kwa Yanga ni kuwa baadhi ya wachezaji waliokuwa na majukumu katika timu za Taifa, wanatarajiwa kurejea kuanzia leo

Kiungo Khalid Aucho raia wa Uganda na mlinda lango Djigui Diarra raia wa Mali huenda wakatua pamoja leo baada ya mchezo baina ya Mataifa yao uliopigwa nchini Uganda jana

Mlinzi kiraka Yannick Bangala yeye huenda akarejea kesho Jumatano wakati wachezaji wenye majukumu katika timu ya Taifa ya Tanzania, wanakamilisha leo kwa mchezo dhidi ya Madagascar na huenda wakaingia kambini baada ya mchezo huo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’