Aucho, Djigui watakiwa 'fasta' kambini

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Sep 2021
Aucho, Djigui watakiwa 'fasta' kambini

Wakati Klabu ya Yanga ikicheza mechi nyingine ya ndani ya mazoezi dhidi ya Pan African jana kujiwinda na mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Kocha Mkuu wa klabu hiyo, Nasreddine Nabi, amewataka mastaa wake waliopo timu za taifa nje ya nchi kukwea pipa mara moja pindi tu mechi zitakapomalizika

Afisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, amesema Nabi amewataka wachezaji wake wawili waliopo nje ya nchi kuzitumikia timu zao za taifa, kiungo Khalid Aucho wa Uganda na kipa Djigui Diarra kukwea pia mara moja pindi tu mechi yao itakapomalizika leo

Uganda leo itaikaribisha Mali kwenye mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia nchini Qatar mwakani, na timu hizo zitakutana nchini Uganda baada ya mechi za awali Waganda kulazimisha sare tasa ugenini dhidi ya Kenya na Mali kuichapa Rwanda

"Kwa ujumla maandalizi kuelekea mechi yetu ya kimataifa Jumapili, yanaendelea vizuri na wachezaji wote wapo fiti, hatuna majeruhi yeyote. Kikubwa kocha alichoagiza ni kwa wachezaji wake wawili Aucho na Diarra, kuhakikisha wanaanza safari mara moja baada ya mechi yao ya kesho (leo) kumalizika ili kuwahi kuendelea na maandalizi na wenzao," alisema Bumbuli.

Kuhusu uwezekano wa kupata mechi nyingine ya ndani ama ya kimataifa ya kirafiki kujiandaa na mchezo huo dhidi ya Rivers United, Bumbuli alisema itategemea na maamuzi ya kocha lakini kwa sasa haitawezekana

"Kwa upande wa mechi ya kimataifa ya kirafiki, hilo halipo kabisa kwa sababu siku ni chache haiwezekana kuanza kulishughulikia hasa ukizingatia wachezaji mpaka waanze kupimwa COVID-19 ili kupata kibali, hilo litakuwa ni vigumu, kama umelisikia hizo ni habari za mitaani tu hazina ukweli wowote.

"Lakini kama kocha atakuwa na mahitaji ya kupata mechi nyingine ya kirafiki ya ndani atatafutiwa ila bado hajasema," alisema Bumbuli.

Nyota mwingine Yannick Bangala yeye yuko na timu ya Taifa ya DR Congo ambayo leo itacheza dhidi ya Benin, huenda akawasili nchini ya Jumatano

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’