Djuma ashangazwa na ukubwa wa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Sep 2021
Djuma ashangazwa na ukubwa wa Yanga

Mlinzi wa kulia wa Yanga Shabani Djuma ameeleza kushangazwa na wingi wa mashabiki waliojitokeza uwanja wa Benjamin Mkapa wiki iliyopita katika kilele cha wiki ya Mwananchi

Mlinzi huyo aliyetua Yanga akitokea klabu ya AS Vita, amesema wao kama wachezaji wana deni kubwa kwa mashabiki katika msimu ujao

Amesema wakati yuko DR Congo aliikuwa akiisikia na kuiona Yanga kupitia runinga lakini baada ya kushuhudia umati ulijaza uwanja wa Benjamin Mkapa, amefahamu amejiunga na timu kubwa sana barani Afrika

"Nikwambie, wakati niko DR Congo nilikuwa naisikia na kuiona klabu hii kupitia runinga"

"Lakini kwa sasa nimepata kushuhudia ukubwa wake, ina mashabiki wengi kitu ambacho kama mchezaji kinakupa ishara ya kiu ya mafanikio katika kila ushiriki wa timu"

"Ama kwa hakika hii timu ni kubwa na sisi kama wachezaji yatupasa kufanya mambo mazuri kulingana na ukubwa wake"

"Umati ule nilioushuhudia siku ya utambulisho, si jambo zuri kuwafanya watoke vichwa chini katika mechi muhimu, tutapambana kuwapa furaha," alisema Djuma

Djuma ni miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa kwa gharama kubwa na GSM, mashabiki wakiweka imani kubwa kwake kutokana na uzoefu alionao

Ni mchezai kiongozi ambaye mchango wake utaisaidia Yanga pengine kuweza kufikia malengo yake

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’