Jana Kamati ya Utendaji ya Yanga chini ya Mwenyekiti Dk Mshindo Msolla, ilitangaza kuundwa kwa Kamati mpya ya Mashindano itakayoongozwa na Mwenyekiti Rodgers Gumbo
Kamati hiyo ina wajumbe nane Hamad Islam, Lucas Mashauri, Abdallah Bin Kleb, Davis Mosha na Seif Magari. Wengine ni Injinia Hersi Said, Pelegrinius Rutayunga na Arafat Haji
Wanachama na mashabiki wa Yanga, kwa wingi wao, wamepongeza uundwaji wa Kamati hiyo ambayo imesheheni watu kwelikweli ambao wengine waliwahi kuiheshimisha Yanga katika miaka ya nyuma
Uteuzi huo umeonyesha dhamira ya Yanga msimu huu ni kushinda makombe, hakutakuwa na malalamiko
Kuna benchi bora la ufundi chini kocha Nasreddine Nabi, usajili makini umefanyika kwa kuleta wachezaji wazoefu na wenye kiu ya mataji
Mashabiki wamehamasika kuiunga mkono timu yao, akiongezwa Haji Manara kuongeza 'amsha-amsha'
Yanga imejipanga kila idara kuhakikisha malengo yanafanikishwa na muhimu kurejea ufalme wake katika soka la Tanzania