Tunazidi kuimarika - Nsajigwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Jan 2018
Tunazidi kuimarika - Nsajigwa
Kocha Msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa amewasifu vijana wake kwa kufanikiwa kutinga nusu fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi baada ya kuichapa Taifa ya Jan'gombe mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa Ijumaa usiku.

Ushindi huo umeifanya Yanga kufikisha alama tisa baada ya pia kuzifunga Mlandege (2-1) na JKU (1-0).

Yanga iko nafasi ya pili nyuma ya Singida United ambayo nayo imefuzu hatua ya nusu fainali baada ya kushinda michezo yake mitatu pia.

Singida United inaongoza kundi A ikiwa na alama tisa na tofauti nzuri ya mabao (+6) huku Yanga ikiwa na (+4).

Akizungumza baada ya mchezo wa jana, Nsajigwa amesema Yanga ilianza taratibu michuano hiyo lakini inazidi kuimarika katika kila mchezo.

Nsajigwa kwa kushirikiana na mwenzake Noel Mwandila wamekuwa wakiwapa nafasi wachezaji wote wa kikosi cha Yanga waliosafiri na timu visiwani Zanzibar.

Utaratibu huo umesaidia kufanya kikosi cha Yanga kime imara wakati wote licha ya ugumu wa ratiba ya michuano hiyo ambayo haina muda wa mapumziko kwa wachezaji.

Aidha Nsajigwa amesifu viwango vinavyoonyeshwa na wachezaji wake na amesema kikosi chake kina uwezo wa kutwaa ubingwa kama wataendeleza kiwango walichonacho sasa.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
23h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’