Mshambuliaji wa zamani wa Yanga Michael Sarpong ametimkia Arabuni akijiunga na klabu ya Al Nahda ya nchini Saudi Arabia kwa mkataba wa miaka miwili
Al Nahda inashiriki ligi daraja la pili nchini humo
Katika msimu mmoja aliyoitumikia Yanga, Sarpong alifunga mabao manne kwenye ligi na mabao mawili katika michezo ya kirafiki
Yanga ililazimika kuvunja mkataba wake baada ya kutoridhishwa na kiwango chake
Wakati Sarpong akitua Arabunu, aliyekuwa mlinda lango wa Yanga Farouk Shikhalo anatajwa kuwa mbioni kujiunga na KMC
ADVERTISE HERE