Tukio la Wiki ya Mwananchi lilifana kwelikweli siku ya jana kwa Yanga kuvunja rekodi ya mahudhurio ya mashabiki waliyoiweka mwaka uliopita
Hamasa imekuwa kubwa kwa mashabiki kuelekea msimu mwingine wa mashindano kwa kikosi cha Yanga
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amewarejesha vijana wake kambini kwa ajili ya maandalizi kwa ajili ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Rivers United
Mchezo huo wa hatua ya awali utapigwa Septemba 12, katika uwanja wa Benjamin Mkapa na mechi ya marudiano kupigwa Nigeria Septemba 19, week moja baadae
Kuna matumaini makubwa kwa kikosi cha Yanga msimu huu kitafanya vizuri kutokana na aina ya usajili uliofanyika
Wachezaji wa Yanga wana deni kubwa kwa mashabiki wao, wamejitokeza kwa wingi katika siku ya kwanza ya utambulisho wao
Huu moto walioanza nao mashabiki jana unapaswa kuendelezwa kwa matokeo mazuri uwanjani na sio vinginenvyo