Baada ya 'kutikisa' nchi katika kilele cha wiki ya Mwananchi pale uwanja wa Benjamin Mkapa hapo jana, Msemaji wa klabu ya Yanga Haji Manara amebainisha kuwa alipata ajali mbaya ya gari wakati akirejea nyumbani
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Manara amethibitisha kuwa gari yake iligongwa na kuharibika vibaya huku mwenyewe akinusurika kifo
Mapema leo, Manara alipaswa kushiriki kipindi cha joto la Asubuhi eFM radio lakini hakufika akitaja sababu kuwa ni tukio hilo alilokumbana nalo usiku
"Nawaomba radhi sana EFM kwa kutofika kwenye kipindi asubuhi ya leo kama nilivyoahidi kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu"
"Usiku wa jana nilinusirika na ajali mbaya ya gari baada ya gari yangu kugongwa vibaya na kusababisha kuharibika vibaya"
"Hadi kuja kulala ilikuwa ni mida mibaya ya usiku mkubwa na sikuweza kuamka mapema ili niwahi kipindi chenu alfajiri ya leo saa kumi na Mbili"
"Nawaomba tena radhi nyie na Wasikilizaji na watazamaji wote. Mnisamehe sana na nimejisikia vibaya sana," aliandika Manara
Hata hivyo 'Buggati' yuko salama kabisa akiendelea na majukumu yake mapya katika klabu ya Yanga