Yanga imekata tiketi ya nusu fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi baada ya kuichapa Taifa ya Jan'gombe mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa Ijumaa usiku.
Yanga imeungana na Singida United baada ya timu zote kushinda michezo yao mitatu waliyocheza.
Mabao ya Yanga yaliwekwa kambani na Ibrahim Ajib na Yohana Nkomola. Wawili hao ndio waliongoza safu ya ushambuliaji ya Yanga.
Ajib aliibuka kuwa nyota wa mchezo huo.
Yanga ilitawala mchezo huo kwa muda mwingi ikiwa imara zaidi sehemu ya kiungo iliyoongozwa na viungo mahiri Raphael Daudi na Edward Maka.
Kinda Said Musa alin'gara kwenye wingi ya kulia akiwa mchezaji aliyefanyiwa madhambi mara nyingi zaidi katika mchezo huo.
Baadae alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Juma Mahadhi.
Katika kikosi cha leo kocha Msaidizi Shedrack Nsajigwa alifanya mabadiliko madogo kwa kuwatumia Pato Ngonyani kama beki wa kulia na Said Juma Makapu kama mlinzi wa kati.
Wawili hao waliweza kumudu vyema nafasi hizo mpya!
Yanga imebakisha michezo miwili dhidi ya Zimamoto na Singida United.

ADVERTISE HERE