Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mh Jerry Muro amewakaribisha viongozi na mashabiki wa Simba kujiunga na Yanga kwani hiyo ndio timu ya Wananchi
Muro ambaye amewahi kuwa Afisa Habari wa Yanga, jana aliongoza Mashabiki na Wanachama wa Yanga katika wilaya yake ya Ikungo kutoa misaada mbalimbali kwa watu wenye mahitaji
Muro alisema Yanga inaendelea kupokea wageni kama walivyompokea Haji Manara ambaye amerejea nyumbani
"Manara kaja Yanga kanenepa, kapendeza, kanawili, afya yake ya akili na mwili imekuwa tofauti. Yanga ndio sehemu pekee ambayo ukitaka burudani ya mpira, ukitaka burudani ya maneno, usajili unakuja Yanga"
"Sisi Yanga tuko tayari kuwapokea wote, akiwemo Mohammed Dewji, tuko tayari kumpokea Barbara, wakati Yanga itakapokuwa bingwa wa Afrika Mo lazima aje kwetu kutangaza biashara zake," alitamba Muro