Mkurugenzi wa Mashindano Yanga Thabit Kandoro amesema kuwa wamewasiliana na TFF kuwaombea ruhusa wachezaji walio kwenye timu ya Taifa ili waweze kushiriki kilele cha wiki ya Mwananchi kesho Jumapili
Baada ya utambulisho wa kikosi hapo kesho, Yanga itacheza mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya Zanaco ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Wachezaji nane wa Yanga wameitwa timu za Taifa, ambapo Diarra Djigui, Mukoko Tonombe na Khalid Aucho wao wamesafiri kujiunga na mataifa yao wakati Ramadhani Kabwili, Dickson Job, Bakari Nondo, Zawadi Mauya na Feisal Salum wako nchini kwenye kambi ya timu ya Taifa kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya DR Congo
"Tumeshaongea na uongozi wa timu ya taifa ya Tanzania juu ya kuwaomba wachezaji wetu wote katika mchezo wa kilele cha siku ya Mwananchi dhidi ya Zanaco FC na tayari ombi letu limekubaliwa," alisema Kandoro